Ukaribisho
Dkt. Alex Ernest
Mganga Mfawidhi wa Hospitali
Karibu katika Tovuti ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru) kwa huduma bora na za kibingwa kutoka kwa madaktari wabobezi
Tunatumaini utapata taarifa za kuaminika unazozihitaji kwa ukamilifu kuhusu wigo, upeo wa taasisi, dira, dhamira, malengo, mikakati na Huduma tunazozitoa.
Mategemeo yetu ni kukupatia huduma unayostahili bila kujali tabaka lolote la Dini, Kabila, Kipato, Rangi, Jinsia, Umri na Taifa unalotoka. Mteja wetu tutamuhudumia kwa kufuata weledi wa kutoa huduma, miongozo na taratibu za nchi kwa kusimamia usawa na haki.
Tovuti hii inamilikiwa na Ofisi ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha. Karibuni sana