Occup therapy clinic

IDARA YA OCCUPATIONAL THERAPY 

MUHTASARI

Idara ya occupational therapy katika hospitali ya rufaa ya mkoa Mt Meru ,inatoa huduma ya utengamao kwa watoto wenye changamot za ukuaji zinazoweza kupelekea kupata ulemavu wa kudumu pamoja na kuwawezesha watotot waliopata ulemavu kuwapa ujuzi na uwezo wa kujimudu na kujihusisha katika shughuli za kila siku.


HUDUMA ZITOLEWAZO

  1. Uchunguzi wa awali kwa watoto wenye changamoto za ukuaji.
  2. Elimu kwa wazazi /jamii jinsi ya kutambua, kuelewa na kuwasaidia watoto wenye changamoto za ukuaji.
  3. Tiba kwa vitendo/shughuli maalumu za kuwajengea watoto uwezo wa kujimudu na kujitegemea.
  4. Kuwezesha na kukuza ukuaji na maendeleo bora ya hisia zinazoratibisha ukuaji.
  5. Ushauri nasaha kwa makundi rika.

SIKU ZA KLINIKI


Jumatatu

  8:00asubuhi– 3:30jioni

 Jumanne

8:00asubuhi– 3:30jioni

Jumatano

8:00asubuhi– 3:30jioni

 

Kupitia idara ya occupational therapy, watoto wenye changamoto za ukuaji wanawezeshwa  kukuza uelewa wao kimwili ,kiakili na hisia kwa vitendo ili kuwawezesha kujimudu vyema kuzuia ulemavu na kwa waliopata ulemavu kuzuia usiendlee.