Ununuzi na Ugavi

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha ina maafisa Ugavi wanaotekeleza mipango ya manunuzi ya Hospitali kwa kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni za Manunuzi ya Umma. Katika kutekeleza sheria hii ya manunuzi, lazima suala la uwazi, uwajibikaji na uadilifu lizingatiwe katika michakato yote ya manunuzi itakayofanywa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.  Hospitali yetu inalazimika kuandaa mpango wa manunuzi unaotokana na mpango wa uendeshaji ulioidhinishwa wa kila mwaka (CHOP)

MAJUKUMU YA KITENGO

  1. Kusimamia shuguli za taasisi nunuzi ( Hospitali ya Mkoa)  ikiwemo manunuzi ya vifaa, huduma na ujenzi  kwa njia sahihi zilizo idhinishwa kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013
  2. Kusaidia kazi za Bodi ya Zabuni.
  3. Kutekeleza maamuzi na maelekezo ya Bodi ya Zabuni na Kuwa sekretariet katika vikao vya Bodi ya Zabuni.
  4. Kuandaa nyaraka za zabuni kwa mujibu wa miongozo ya PPRA.
  5. Kuandaa matangazo ya Zabuni.
  6. Kuandaa mikataba ya Zabuni ya Hospitali ya Mkoa na pia kupitia mikataba ya manunuzi ya iliyo andaliwa kwa kufuata miongozo ya PPRA.
  7. Kutunza kumbukumbu za michakato ya manunuzi na ufutaji wa vifaa vilivyoisha muda wake (disposal of asset).
  8. Kuandaa na kutunza rejista ya mikataba iliyo sainiwa baina ya Hospitali na wadau wa manunuzi.