Huduma ya Tiba na Afya ya Mtoto

Karibu kwenye Idara ya Watoto;-

Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mt Meru. Nia yetu ni kutoa huduma bora kwa wagonjwa wetu na kuhakikisha watoto na Wazazi/Walezi wao wanafurahia maisha bora.

Tunatoa huduma kwa wagonjwa na nje na wa ndani

A. Huduma za Wagonjwa wa Nje 

Tuna kliniki kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa

 Jumatatu: Kiliniki ya watoto wachanga

Alhamis: Kliniki ya watoto na vijana wanaoishi na VVU

Jumanne: Kliniki ya magonjwa yote

Ijumaa: Kliniki ya watoto wenye kisukari

Jumatano: Kliniki ya watoto na vijana wanaoishi na virusi vya ukimwi (VVU)

Jumamosi (mara moja kila mwezi): kliniki ya vijana wanaoishi na VVU


B. Huduma za Wagonjwa wa Ndani

Idara ina vitengo vitatu (3): 1) Kitengo cha watoto waliozidiwa na  wanaohitaji uangalizi maalum ; 2) Kitengo cha magonjwa yote kwa ujumla; na 3) Kitengo cha watoto wachanga.

Kitengo cha watoto waliozidiwa na  wanaohitaji uangalizi maalum

Kitengo hiki hushughulika na watoto wagonjwa wenye hali ambayo inahitaji ufuatiliaji wa karibu. Hali hizi ni kama vile viungo kushindwa kufanya kazi, kisukari, kukosa fahamu, kunywa sumu, na kubanwa kifua. Watoto hufuatiliwa katika Kitengo hiki mpaka wawe imara. Kisha huhamishiwa kwenye kitengo cha magonjwa yote kwa ujumla.

Kitengo cha magonjwa yote kwa ujumla

Kitengo hiki kimegawanywa katika sehemu 3:-

  1. Moja: watoto wenye magonjwa mbalimbali
  2. Mbili: watoto wenye magonjwa sugu na waliopata nafuu na wanamalizia dawa
  3. Tatu ni Utapiamlo: watoto wenye utapiamlo mkali hulazwa huku kwa matibabu ya awali

Kitengo cha Watoto Wachanga

Kitengo hiki ni kwa ajili ya watoto wachanga wenye umri kati ya siku 0 hadi 28. Kitengo kimegawanywa katika:

  • Sehemu ya huduma ya watoto wachanga walizidiwa
  • Sehemu ya huduma kwa watoto waliozaliwa kabla ya wiki 36 (njiti), na wale waliozaliwa na uzito mdogo
  • Kangaroo Mother Care: watoto waliozaliwa na uzito mdogo hukaa na mama zao katika chumba hiki kabla ya kuruhusiwa
  • Sehemu ya huduma kwa watoto wenye maambukizi: sehemu hii ni kwa ajili ya kutibu watoto wenye maambukizi
  • Sehemu ya uangalizi: Watoto wa kawaida huletwa kwa ajili ya uangalizi wa muda aidha kwa sababu mama ni mgonjwa au hayupo kabisa
  • Sehemu ya Mionzi kwa ajili ya watoto wenye manjano kwenye macho na ngozi