Huduma za Uchunguzi

IDARA YA RADIOLOJIA

Huduma zitolewazo:-

Utambuzi wa magonjwa (maradhi) mivunjiko, Miteguko na Hitilafu mbalimbali za viungo vya mwili kwa kutumia mashine maalumu zinazotoa mionzi za kisasa (x-ray) na mashine za mawimbi ya sauti na za kisas (ultrasound);-

  1. Tunatoa huduma zote za x-ray za kawaida. Mfano;- X- Ray za miguu, magoti, mifupa ya paja, mikono,mabega,kifua,nyonga ,uti wa mgongo na kichwa.
  2. tunatoa huduma za upimaji wa viungo vya ndani ya nyonga, tumbo na vichwa (kwa watoto wachanga).
  3. vilevile tunafanya vipimo maalumu vya upimaji wa maziwa/matiti, goita, korodani, vivimbe na tezi dume.

Masaa ya kazi;

SIKU SIKU ZA KAWAIDA HUDUMA ZA DHARURA
Jumatatu - ijumaa 01:30 Asubuhi - 09:30 Alasiri Masaa 24
siku za 'weekend & public' (Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu)
Masaa 24