utawala na rasilimali watu

SEKSHENI YA UTAWALA NA RASILIMALI WATU

Seksheni hii ina lengo la kuziwezesha Seksheni nyingine kutimiza majukumu yake, kutoa utaalamu na huduma mbalimbali zinazohusiana na usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala kwenye Hospitali ya Mkoa (Mount Meru). Seksheni inawajibika kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali.

Majukumu ya Seksheni ya Utawala na Rasilimali watu:

  1. kuratibu masuala ya Mahusiano na Ustawi wa Wafanyakazi ikiwa na pamoja na masuala ya Afya, Usalama, Michezo na Utamaduni.

  2. kuratibu maandalizi, utekelezaji, usimamizi na tathimini ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja kwenye Hospitali ya Mkoa.

  3. kutoa huduma za Masijala, Ofisi na utunzaji na usimamizi wa kumbukumbu.

  4. kuratibu huduma za Ulinzi, Usafi na utunzaji Ofisi, majengo na maeneo/viwanja..

  5. Kutoa huduma za ujumla za uangalizi wa vifaa vya ofisi na majengo.

  6. Kuratibu utekelezaji wa jukumu la kuimarisha Nidhamu ikijumuisha utoaji wa elimu ya kuzuia Rushwa..

  7. Kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma – Tume/Sekretarieti ya Ajira juu ya masuala yote yanayohusiana na Ajira na Uteuzi wa watumishi.

  8. Kusimamia hatua/Mchakato wa kuwathibitisha na kuwapandisha vyeo/madaraja watumishi wa Hospitali