Maabara

Posted on: June 19th, 2024

Maabara ni idara mojawapo kati ya idara zilizopo katika Hospitali ya Mount Meru. Idara hii inasimamia vitengo vifuatavyo;-

  • Bacteriology
  • Blood Transfusion
  • Chemistry
  • Haematology
  • Parasaitology na
  • Serology

Maabara ya hospitali hii imepata Ithibati ya kimataifa (ISO15189/2012) na kuifanya iwe maabara ya Hospitali ya Mkoa ya kwanza nchini Tanzania kufikia hatua hiyo.

Maabara hii inauwezo wa kufanya vipimo vyote kwa kutumia vifaa na mashine za kisasa kabisa. Baadhi ya vipimo hivyo ni pamoja na vipimo vya uchunguzi wa magonjwa, kama vipimo vya damu (FBP),mkojo. Pia vipimo vya ini na figo vinafanyika lakini pia upimaji na ubainishaji wa vidudu mbalimbali kwa kutumia Teknolojia ya  Microbilojia.

Pia ubainishaji wa maambukizi ya magonjwa ya UKIMWI, na uwingi wa Virusi inafanyika.

Masaa ya kazi

Siku Siku za kawaida Huduma za Dharura
Jumatatu mpaka Ijumaa

01:30Asubuhi - 09:30Alasiri

Masaa 24
mwisho wa siku za wiki (jmosi &Jumapili) na siku za sikukuu
Masaa 24