ZIARA YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA KUKAGUA MITUNGI YA GESI YA OKSJENI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA AUSHA (MOUNT MERU)

Posted on: July 12th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amefanya ziara katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Wilaya ya Arusha mjini kukagua mitungi ya gesi ya oksjeni kama moja ya njia za kukabiliana na matibabu ya  wagonjwa wenye changamoto wa mfumo wa upumuaji ambao idadi yao inaongezeka kila siku.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Mkoa wa Arusha (Mount Meru) Dr.Alex Ernest alisema mitungi ya oksjeni iliopo hospitali kwa sasa inajitosheleza kulingana na wagonjwa waliopo na wanaoendelea kupatiwa matibabu.

Ziara iyo ya Mkuu wa Mkoa alioambatana na Mkuu wa Wilaya wa  Jiji la Arusha Mhe. Sofia Mjema walijiridhisha na hali ya hospitali kukabiliana na uwezo wa kutoa matibabu kwa wagonjwa wenye changamoto kwenye mfumo wa upumuaji  kwa kukagua vifaa na mitungi ya gesi itakayosaidia kwenye zoezi  lakutoa matibabu.