TAARIFA KWA UMMA
Posted on: September 2nd, 2021Zoezi la utoaji chanjo linaendela katika kituo cha Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru, kila siku.
Wananchi walio tayari kuchanja wanapaswa kujisajili taarifa zao kupitia: chanjocovid.moh.go.tz, na kufika kituoni kwa ajili ya kuchanja.
Aidha, Vyeti vya Kielektroniki vimeanza kutolewa na yeyote ambaye amepata Chanjo ya UVIKO-19 anapaswa kurudi katika Kituo alipopatia Chanjo kusajiliwa taarifa zake na kupatiwa cheti hicho.