Chanjo ya Polio,Surua na Rubela

CHANJO YA POLIO,SURUA-RUBELA SASA YAPATIKANA MOUNT MERU HOSPITAL.

Chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio, Surua-Rubela sasa inapatikana Mt Meru RRH Hivyo Wazazi na walezi wanatakiwa Wawalete watoto wenye umri wa miezi tisa mpaka miaka mitano, kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio, Surua-Rubela kwa kuwa chanjo hizo zinaokoa maisha ya watoto pamoja na kuokoa gharama kubwa ,ambazo familia na taifa ingezitumia kwa kutibu magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa kinga chanjo. 

- 21 September 2019