TAARIFA KUHUSU COVID19

TAARIFA KWA UMMA

Uongozi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha- Mount Meru inapenda kuwataarifu wateja wake na Umma kwa ujumla kuhusiana na vita dhidi ya magonjwa ya  mlipuko bado inaendelea. Hospitali inachukua fursa hii kuwakumbusha wananchi kuzingatia  tahadhari iliotolewa hivi karibuni na  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  kusisitiza tamko lililotelewa na Rais wetu Mhe.Samia Suluhu Hassan kuwa Wananchi waendelee kuchukua tahadhari za kujikinga dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 ambao dunia imeendelea kupambana na mawimbi ya mlipuko wa ugonjwa huu.

Hivyo Hospitali inawakumbusha Wananchi wote kutopuuza ugonjwa huu wa Covid-19 na jukumu la kujikinga dhidi ya ugonjwa huu ni la kila mmoja wetu, hivyo tusiwe na hofu ila tuendelee kuzingatia hatua za kujikinga ambazo ni:

  • Safisha mikono yako mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kwa dawa ya kutakasa mikono.
  • Epuka kusalimiana Kwa kushikana mikono.
  • Funika mdomo na pua wakati wa kukohoa au kupiga chafya.
  • Epuka kugusa macho, pua au mdomo.
  • Kaa umbali wa angalau zaidi ya mita moja kati yako na mtu mwingine.
  • Epuka misongamano.

Vilevile Hospitali inapenda kutoa utaratibu unaoendelea  wakuona wagonjwa wodini mtu mmoja ataruhusiwa kuingia wodini kwa kila mgonjwa aliopo wodini lengo kuu ni kuzuia msongamano unaoweza kujitokeza wodini na kuvaa Barakoa kipindi chote unapokuwa eneo la Hospitali.

Aidha Uongozi wa Hospitali unauhakikishia Umma kuwa Hospitali itaendelea kutoa huduma bora kwa Wananchi wote bila kuchoka na kwa wakati wote.

- 12 July 2021